Shilole ateswa na wanaume
Msanii wa bongo fleva, Zuwena Mohamed alimaarufu kama Shilole amefunguka zile tetesi za yeye kubadilisha wanaume kama nguo na kusema siyo kweli kwamba yeye anapenda kufanya hivyo ila wanaosababisha yote hayo ni wanaume wenyewe kutotulia. Shilole amebainisha hayo kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa Facebook ya EATV, Shilole baada ya kuulizwa swali na shabiki alidai kuwa yeye anapenda sana kutulia ila wanaume ambao huwa anawapata ndiyo huwa hawatulii jambo ambalo linamfanya yeye aonekane hajatulia. "Sisi wanawake inapotokea upo katika mahusiano halafu ukaachana na mtu huyo unaonekana 'malaya' lakini kumbe siyo kweli wakati mwingine mtu unakuwa unashindwa kuvumilia matatizo ya mahusiano ukaamua kutoka kwenda kwa mwingine kwa kuwa siyo ndoa sasa ya nini niendelee kuteseka katika mahusiano". Alisema Shilole Mbali na hilo Shilole amesema kuwa amekuwa na bahati mbaya sana kwenye mahusiano kwani m...