DKT. SAMIA KUKABIDHI HUNDI YA SHILINGI BIL.16 KWA WATAFITI 16 WA MABADILIKO YA TABIA NCHI.
DKT. SAMIA KUKABIDHI HUNDI YA SHILINGI BIL.16 KWA WATAFITI 16 WA MABADILIKO YA TABIA NCHI.
#KAZIINAONGEA
Katika kuwathamini wabunifu wa ndani, Rais. wa awamu ya sita, Dkt.Samia Suluhu Hassan, anatarajia kukabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 6.3 kwa watafiti 16 katika masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa kuzingatia umuhimu wa kuhimili mabadiliko ya Tabia nchi na kukuza uchumi shindani, STICE ya mwaka huu inaonyesha jinsi bunifu za ndani zinavyoweza kuleta maendeleo endelevu.
Rais Dkt. Samia anatarajia kukabidhi hundi hiyo wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa Mikopo wa kusaidia ubidhaishaji na ubiasharaishaji wa ubunifu na teknolojia zinabuniwa na vijana wa Kitanzania.
Akielezea kuwepo kwa Kongamano hilo la tisa la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema, kongamano hilo linatarajia kufanyika kuanzia Desenba 2 hadi 4, 2024.
Mfuko huo unaanza na kiasi cha Shilingi Bilioni 2.3 ambazo zitatumika kukopesha wabunifu kuendeleza kazi zao.
Katika kongamano hilo pia Rais anatarajia kuwatambua na kutoa tuzo kwa wanasayansi na wabunifu ambao matokeo ya kazi zao zimechangia kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii ndani na nje ya nchi.
#KAZIINAONGEA

Comments
Post a Comment