Posts

Showing posts from May, 2017

Shilole ateswa na wanaume

Image
Msanii wa bongo fleva, Zuwena Mohamed alimaarufu kama Shilole amefunguka zile tetesi za yeye kubadilisha wanaume kama nguo na kusema siyo kweli kwamba yeye anapenda kufanya hivyo ila wanaosababisha yote hayo ni wanaume wenyewe kutotulia. Shilole amebainisha hayo kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa Facebook ya EATV, Shilole baada ya kuulizwa swali na shabiki alidai kuwa yeye anapenda sana kutulia ila wanaume ambao huwa anawapata ndiyo huwa hawatulii jambo ambalo linamfanya yeye aonekane hajatulia. "Sisi wanawake inapotokea upo katika mahusiano halafu ukaachana na mtu huyo unaonekana 'malaya' lakini kumbe siyo kweli wakati mwingine mtu unakuwa unashindwa kuvumilia matatizo ya mahusiano ukaamua kutoka kwenda kwa mwingine kwa kuwa siyo ndoa sasa ya nini niendelee kuteseka katika mahusiano". Alisema Shilole Mbali na hilo Shilole amesema kuwa amekuwa na bahati mbaya sana kwenye mahusiano kwani m...

Afande Sele ampa makavu Msanii Wakazi

Image
Mwanamuziki mkongwe wa Hip Hop Tanzania Afande Sele amesema kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM akidai kuwa hamjui msanii wa Hip Hop Wakazi baada ya msanii huyo kuwataja wasanii wanaoandika mashairi na kusema Afande Sele hayupo technically. Baada ya kauli hiyo ya Wakazi, Afande Sele aliitumia account yake ya Twitter akiandika kuwa hamjui Wakazi kabla ya leo May 3, 2017 kuirudia kauli hiyo kupitia 255 akisema: “Naapa mbele za Mungu kwamba Wakazi simfahamu kwa sura na sijawahi kumuona. Kazi zake sijawahi kuzisikiliza, isipokuwa jana jioni mshikaji mmoja alinikumbusha na kusema alishawahi kuimba kama Mangwea. Kwa hiyo, alijivisha umangwea baada ya kufariki, ila sijui kazi yake hata moja. “Kuna kipindi nilijitoa kwenye Group ambalo tulikuwa wote, kwa sababu anajifanya anajua kila kitu wakati hajui kitu chochote. Sasa sioni kama kuna tija yoyote ya yeye kuniona labda mimi nafanya nini maana ...

Nitajiuzulu kwa uamuzi wa wananchi: Maalim Seif

Image
Dar  es Salaam. Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif  amesema yuko tayari kujizulu siasa na kuwapisha wengine iwapo wananchi watamwomba kufanya hivyo. Maalim Seif ambaye yuko katika ziara isiyo rasmi jijini Dar es salaam amesema hayo leo (Jumatano) katika mahojiano kwenye kipindi cha 360 kinachorushwa na Clouds tv kila siku za wiki. Amesema anaamini katika siasa za mshikamano unaoundwa na wananchi hivyo iwapo wananchi hao wataona muda wake wa kutumika kwenye siasa unatosha basi atatii ridhaa yao na kujiweka kando. “Suala la kujiuzulu siyo jambo la ajabu…mimi najua napendwa na wananchi tena napendwa kweli. Jambo moja kuwa iwapo wakisema sasa inatosha niondoke nitafanya hivyo,” amesema Maalim Seif.

Dk Mwakyembe: Televisheni, Redio kusoma vichwa vya habari tu kwenye magazeti kuanzia kesho

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe   Mwanza.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amezitaka Televisheni na Redio kuanzia kesho kusoma vichwa vya habari vya magazeti tu ili kuwavutia wasomaji kununua magazeti kwa habari kamili. Dk Mwakyembe amesema hayo leo jijini Mwanza katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini ambapo pia amesema ataendelea kutetea na kulinda haki za waandishi wa habari huku akiwahakikishia ulinzi waandishi wa habari za uchunguzi. Pamoja na mambo mengine Dk Mwakyembe amehakikisha kuwepo kwa ushirikiano wa kutosha kwa wamiliki wa vyombo vya habari  na kwamba ameagiza idara ya mawasiliano kutengeneza mawasiliano ya kudumu na wawe wanakutana angalau mara moja kwa mwezi kujadili udhaifu unaoweza kujitokeza

Tunduma kumekucha kwa happy birthiday

Image
sherehe hii ilifanyika mjini Tunduma na ilifana sana yaani ilikuwa kama kingodoro watu walijiachia sana hadi ikafikia hatua ya kujisahau