Posts

RAIS SAMIA AWAONGOZA WATANZANIA KUMUAGA DKT. NDUGULILE

Image
 RAIS SAMIA AWAONGOZA WATANZANIA KUMUAGA DKT. NDUGULILE #KAZIINAONGEA Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Desemba 2, 2024 ameshiriki Ibada ya kuuaga mwili wa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya duniani (WHO) kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile. Shughuli ya kumuaga mwanasiasa huyo imefanyika kwenye viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam na Rais Dkt. Samia pia amesaini kitabu cha Maombolezo.

ELIMU BILA MALIPO MSAADA KWA WATANZANIA WENGI

Image
ELIMU BILA MALIPO MSAADA KWA WATANZANIA WENGI #KAZIINAONGEA Serikali ya Awamu ya Sita iliyo chini ya kiongozi mwenye dhamira ya kumwondolea umasikini Mtanzania, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanikisha kuendeleza utoaji wa huduma ya elimu ya msingi bila malipo, hali iliyowawezesha Watanzania wengi kupeleka watoto wao shule. Ikumbukwe kuwa dhana ya Elimumsingi Bila Malipo inawezesha utoaji wa Elimu kwa Mwanafunzi yeyote bila Mzazi au Mlezi kulipa ada wala michango ya fedha katika shule.  Utozaji wa ada au michango mbalimbali shuleni kwa mwanafunzi ilikuwa ni kikwazo kikubwa hasa kwa Wazazi au Walezi wasio na uwezo. Kikwazo hicho kilisababisha baadhi ya wanafunzi wasiolipa michango au ada kutohudhuria au kuacha Shule.   Katika kipindi cha kuanzia April, 2021 hadi Februari, 2024 jumla ya Shilingi Trilion 1.1 zimetolewa na Serikali ya Awamu ya Sita na kutumwa Shuleni kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango wa Elimumsingi Bila Malipo.  Fedha hizo ni kwa ajili ya ruzuku ya uendeshaji shule, fe...

MTWARA, LINDI ZAINGIZWA KWENYE GRIDI YA TAIFA

Image
MTWARA, LINDI ZAINGIZWA KWENYE GRIDI YA TAIFA  #KAZIINAONGEA Serikali inatekeleza mradi wa umeme Gridi ya Taifa  kwa kuiunganisha mikoa ya Mtwara na Lindi kutokea Songea kwa kupitia njia ya Tunduru, Masasi -Mahumbika. Hii ni  kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Nishati Bungeni Jijini Dodoma Novemba 4, 2024. Aidha Wizara ya Nishati inatekeleza agizo la Rais Dkt Samia  Suluhu Hassan la kutaka kuwalipa fidia wananchi wote waliopisha mradi wa kuunganisha umeme kwenye Gridi ya Taifa kwenda mikoa ya Mtwara na Lindi. #KAZIINAONGEA

DEREVA ASHIKILIWA KWA KUSABABISHA KIFO CHA ASKARI SONGWE

Image
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linamshikilia dereva wa Gari yenye namba za usajll T.633 ECF aina ya Toyota Rumio aitwaye Ombeni Evarist Sanga (30) mfanyabiashara na mkazi wa Mji mdogo wa Tunduma kwa kosa la kuendesha Gari kwa uzembe kisha kuacha njia, kupinduka na kusababisha kifo kwa Askari WP.1 1725 Koplo Leokadia,. Ni kwamba Novemba 10, 2024 saa 8:15 usiku eneo la Old Vwawa, Tarafa ya Vwawa, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe katika barabara ya Mbeya Tunduma, Gari namba T.633 ECF aina ya Toyota Rumio iliyokuwa ikiendeshwa na Ombeni Evarist Sanga (30) akitokea Tunduma kuelekea Vwawa iliacha njia, kupinduka na kusababisha kifo kwa askari Polisi Namba WP.11725 Koplo Leokadia Nestory Mwenda Aidha, katika ajali hiyo, Askari mwingine namba WP.11533 Koplo Tabia alijeruhiwa na kwa sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Songwe. Uchunguzi umebaini kuwa chanzo cha ajali ni uzembe wa Dereva kushindwa kulimudu Gari kutokana na mwendo kasi.

RAIS SAMIA AMLILIA MAFURU

Image
RAIS SAMIA AMLILIA MAFURU ● Atuma Salamu za pole Tume ya Mipango. #KAZIINAONGEA Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemtumia salamu za rambirambi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof.Kitila Mkumbo, kufuatia kifo cha aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Marehemu Lawrence Nyasebwa Mafuru. Marehamu Mafuru amefariki Novemba 9 2024, katika Hospitali ya Apollo nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu. Rais Dkt. Samia anatoa pole kwa Watumishi wa Tume ya Mipango, ndugu jamaa na marafiki kufuatia msiba huo. Marehemu Mafuru atakumbukwa kwa Utumishi wake uliotukuka, bidii na ubunifu alipotumikia nafasi mbalimbali ndani za Serikali. #KAZIINAONGEA

SERIKALI YAENDELEA KUJENGA SHULE 100 ZA AMALI NCHINI

Image
SERIKALI YAENDELEA KUJENGA SHULE 100 ZA AMALI NCHINI #KAZIINAONGEA Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema, tayari ujenzi wa shule 100 za Amali ufundi umeanza katika mikoa mbali mbali nchini. Ujenzi wa shule hizo za Amali ni moja ya vipaumbele vya Serikali ya Dkt. Samia, kuhakikisha wanafunzi wakimaliza kidato cha nne, watakuwa na uwezo wa kuajiriwa, kujiajiri na kuajiri. Matarajio ya vijana wengi wanaosoma ni wanapomaliza kupata elimu ni kupata ajira na watoto ni wengi sana wote wanasoma kwa matarajio ya kupata ajira. Prof. Mkenda amesema, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetoa maagizo kwa Wizara ya Elimu, kuweka msukumo wa mafunzo ya Amali Uhandisi yanayojikita kwenye ujuzi zaidi. Shule hizo 100 zinazoendelea kujengwa nchini, zitaweka msukomo katika kutoa Elimu ya Michezo, Utalii, Kilimo, Uvuvi, Ufundi Umeme, Uashi na Useremala. Ujenzi wa Shule hizo za Amali, utapewa kipaumbele katika maeneo ambayo hayana Vyuo vya Ma...

SHILINGI BILIONI 114 ZAFANIKISHA MRADI WA MAJI MANYARA

Image
SHILINGI BILIONI 114 ZAFANIKISHA MRADI WA MAJI MANYARA # KAZIINAONGEA Katika kuendelea na Kampeni yake ya kutokemeza tatizo la Maji nchini, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 114 kwa ajira ya kufikisha maji kwa Wananchi Mkoani Manyara. Kiasi hicho cha fedha kimetolewa ikiwa ni kutekeleza kampeni ya kuondoa tatizo la maji nchini. Mafanikio hayo ya Miradi ya Maji, yameweza kuwafikia Wananchi waliokuwa wanakabiliwa na uhaba wa maji Mkoani  Manyara. Miongoni mwa fedha hizo, Shilingi Bilioni 89.7 zilitolewa kwa ajili ya Miradi ya maji vijijini, Shilingi Bilioni 24.4 kwa ajili ya Miradi ya Maji Mijini. Katika kipindi cha miaka mitatu, Serikali kupitia Mradi wa Mfuko wa Maji (NWF), imewezesha maeneo yaliyokuwa yanakabiliwa na uhaba wa maji, kuweza kupata huduma hiyo. #KAZIINAONGEA