ELIMU BILA MALIPO MSAADA KWA WATANZANIA WENGI
ELIMU BILA MALIPO MSAADA KWA WATANZANIA WENGI #KAZIINAONGEA Serikali ya Awamu ya Sita iliyo chini ya kiongozi mwenye dhamira ya kumwondolea umasikini Mtanzania, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanikisha kuendeleza utoaji wa huduma ya elimu ya msingi bila malipo, hali iliyowawezesha Watanzania wengi kupeleka watoto wao shule. Ikumbukwe kuwa dhana ya Elimumsingi Bila Malipo inawezesha utoaji wa Elimu kwa Mwanafunzi yeyote bila Mzazi au Mlezi kulipa ada wala michango ya fedha katika shule. Utozaji wa ada au michango mbalimbali shuleni kwa mwanafunzi ilikuwa ni kikwazo kikubwa hasa kwa Wazazi au Walezi wasio na uwezo. Kikwazo hicho kilisababisha baadhi ya wanafunzi wasiolipa michango au ada kutohudhuria au kuacha Shule. Katika kipindi cha kuanzia April, 2021 hadi Februari, 2024 jumla ya Shilingi Trilion 1.1 zimetolewa na Serikali ya Awamu ya Sita na kutumwa Shuleni kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango wa Elimumsingi Bila Malipo. Fedha hizo ni kwa ajili ya ruzuku ya uendeshaji shule, fe...