RAIS SAMIA AMLILIA MAFURU
RAIS SAMIA AMLILIA MAFURU
● Atuma Salamu za pole Tume ya Mipango.
#KAZIINAONGEA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemtumia salamu za rambirambi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof.Kitila Mkumbo, kufuatia kifo cha aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Marehemu Lawrence Nyasebwa Mafuru.
Marehamu Mafuru amefariki Novemba 9 2024, katika Hospitali ya Apollo nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.
Rais Dkt. Samia anatoa pole kwa Watumishi wa Tume ya Mipango, ndugu jamaa na marafiki kufuatia msiba huo.
Marehemu Mafuru atakumbukwa kwa Utumishi wake uliotukuka, bidii na ubunifu alipotumikia nafasi mbalimbali ndani za Serikali.
#KAZIINAONGEA

Comments
Post a Comment