DEREVA ASHIKILIWA KWA KUSABABISHA KIFO CHA ASKARI SONGWE
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linamshikilia dereva wa Gari yenye namba za usajll
T.633 ECF aina ya Toyota Rumio aitwaye Ombeni Evarist Sanga (30) mfanyabiashara
na mkazi wa Mji mdogo wa Tunduma kwa kosa la kuendesha Gari kwa uzembe kisha
kuacha njia, kupinduka na kusababisha kifo kwa Askari WP.1 1725 Koplo Leokadia,.
Ni kwamba Novemba 10, 2024 saa 8:15 usiku eneo la Old Vwawa, Tarafa ya Vwawa,
Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe katika barabara ya Mbeya Tunduma, Gari namba
T.633 ECF aina ya Toyota Rumio iliyokuwa ikiendeshwa na Ombeni Evarist Sanga (30)
akitokea Tunduma kuelekea Vwawa iliacha njia, kupinduka na kusababisha kifo kwa
askari Polisi Namba WP.11725 Koplo Leokadia Nestory Mwenda
Aidha, katika ajali hiyo, Askari mwingine namba WP.11533 Koplo Tabia alijeruhiwa na
kwa sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Songwe.
Uchunguzi umebaini kuwa chanzo cha ajali ni uzembe wa Dereva kushindwa kulimudu
Gari kutokana na mwendo kasi.

Comments
Post a Comment